Kikao Kamati Kuu CCM: Wagombea Uwenyekiti wa wilaya za Moshi mjini, Hai, Siha, Makete Musoma Mjini na Vijijini wateuliwa
Kikao Kamati Kuu CCM: Wagombea Uwenyekiti wa wilaya za Moshi mjini, Hai, Siha, Makete Musoma Mjini na Vijijini wateuliwa
IKULU,
DAR: Chama cha Mapinduzi (CCM) leo kimeanza rasmi kikao cha Kamati Kuu
ya chama hicho kinachoongozwa na Mwenyekiti wake Rais John Pombe
Magufuli na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa Chama
cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana akithibitisha kutimia kwa
akidi kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM jijini Dar es
salaam kinachoongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Rais Dkt. John Pombe
Magufuli leo Jumatatu Novemba 20, 2017.
CCM
kupitia Kamati kuu (CC) imefanya uteuzi wa wagombea walioomba kuwania
nafasi ya Uenyekiti katika wilaya Sita nchini zikiwemo zile wilaya za
kichama.
Wilaya
ambazo zimepata wagombea ni Moshi Mjini, Siha na Hai zote za mkoani
Kilimanjaro ambapo uchaguzi umepangwa kufanyika Desemba 1-2 mwaka huu.
Wilaya ya Makete mkoani Njombe pamoja na wilaya zinazotambulika kichama
za Musoma Mjini na Musoma Vijijini mkoani Mara uchaguzi wake umepangwa
kufanyika Novemba 25-26 mwaka huu.
0 Comment: