Leo tunapokea msaada ya mashine 62 za usafishaji Damu kutoka nchi ya Saudi Arabia

Leo tunapokea msaada ya mashine 62 za usafishaji Damu kutoka nchi ya Saudi Arabia, kwetu ni msaada mkubwa maana kumekuwa na ongezeko mkubwa sana wa wagonjwa wa Figo" Naibu waziri wa Afya"Kwa sasa tuna vituo 19 vinavyotoa usafishaji wa figo na vingi vipo Dar es salaam na hii ni huduma ya maisha inahitaji kusafisha kila  Mara,Tunaendelea kuboresha Huduma hizi ziende mikoani karibu na wananchi" Naibu waziri wa afya
 faustine ndugulile


  "Kama serikali mashine Tutazipeleka mikoani kama tanga mwanza,kigoma kagera Iringa pomoja unguja na Zanzibar na  tunaziweka hizi huduma kimkakati kabisa na lengo ni kuzisogezea huduma hizi kwa urahisi kwa mwananchi 
Changamoto sasa ni magonjwa yasiyoambukizwa kama kisukari na Figo,japo Tunajipanga kuzindua mpango wa Taifa wa kupambana na magonjwa haya na Tunayaona hasa kwa vijana jambo ambalo linatupa mashaka"

"Imetusaidia kuokoa fedha za kwenda nje maana ilihitaji zaidi ya milioni 100 kwenda nje, kwa sasa Tuna session zaidi ya 3 pale muhimbili kusafisha figo,na Hadi sasa Tuna mashine 270 Nchi nzima japo bado ni chache sana Lengo ni Tuwe na mashine   kila Hospital ya Rufaa"  

Lengo letu ni Huduma zitolewe na kwa Gharama Nafuu sana ili kila mwananchi aweze kuzimudu kama Nchi za wenzetu wanavyofanya, Tunaamini Tukisogeza Huduma mikoani itakuwa Rahisi kuzipata kwa wananchi wasio na kipato 

0 Comment: