faini ya milioni 5 tanzania mtandao
Sekta ya mawasiliano Tanzania inakua kwa kasi ila hivyo hivyo changamoto za kiusalama zinazidi kuongezeka.
Sambaza

Mapendekezo ya sheria dhidi ya utumiaji usio sahihi wa laini za simu ambazo hazijasajiliwa yamefikishwa bungeni Tanzania.

Mapendekezo hayo yanahusisha ulipwaji wa faini ya sh milioni 5 au kifunge cha miezi 12 jela kwa mtu yeyote atayekamatwa na laini ya simu ambayo haijasajiliwa na ikatumika katika uhalifu/uvunjifu wa sheria.

Katika mapendekezo ya mabadiliko hayo ya kisheria pia mtoa huduma, msambazaji, wakala au mtu yeyote atayasambazi au kusababisha utumiaji wa laini ya simu isiyosajiliwa naye pia atajikuta katika makosa. Kundi hilo litajikuta likipigwa faidi ya hadi milioni 10 au kivungo kisichopungua miaka miwili jela au vyote kwa pamoja.
Malengo ni mazuri, ila kutokana na kiwango cha juu sana cha faini uzembe kidogo unaweza sababisha mamia ya watu kujikuta jela miezi 12 kila mwaka.
Ukiangalia kwa haraka faini ya milioni 5 kwa mtumiaji wa kawaida nchini kuna uwezekano mkubwa akajikuta moja kwa moja kifungoni. Wanaosajili laini wanatakiwa kuwa makini ili kuhakikisha mteja na wao wenyewe hawajikuti katika matatizo.
Ni mategemeo yetu wabunge kujaribu kushusha kiwango hichi cha faini ili kuhakikisha wananchi wa kawaida kuweza kumudu faini pale watakapojikuta katika matatizo kama haya.

Vipi wewe una mtazamo gani juu ya mapendekezo haya?