JUMUIA YA WAZAZI MKOANI KAGERA WAWATAKA WAZAZI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUPAMBANA NA MIMBA ZA UTOTONI.

JUMUIA YA WAZAZI MKOANI KAGERA WAWATAKA WAZAZI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUPAMBANA NA MIMBA ZA UTOTONI.



Jumuiya ya Wazazi kupitia Chama cha Mapinduzi Ccm Mkoani Kagera imewataka Wazazi kushirikiana ipasavyo  kutoa taarifa sahihi kwa vyombo vya Dola pale anapobainika mtu yeyote aliyehusika kumfanyia vitendo vya  kikatili Mtoto  ikiwemo ya kuumpa ujauzito mwanafunzi.  Wito huo umetolewa hii leo na  Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa  wa Kagera Angelus Wilbad Kamugisha  wakati akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake.    Kamugisha amefafanua kuwa  kumekuwepo na changamoto ya matukio kadhaa kwa  baadhi ya  watoto wanaokatishwa masomo baada ya kupata mimba   katika maeneo mbalimbali ya Wilaya za Mkoa huo, ambapo ametolea mfano Halmshauri ya Wilaya ya Ngara kuonekana ikiongoza juu ya  watoto  wanaopata mimba hususani wanafunzi huku  akivitaja baadhi ya vyanzo vinavyochochea  ongezeko  la vitendo hivyo kuwa ni pamoja na kuporomoka kwa maadili katika jamii, tamaa, sambamba na Wazazi kushiriki kuwalinda na kutotoa taarifa sahihi kwa vyombo vya Dola ikiwemo Mahakama pale  vinapokuwa vimewatia mbaroni  watu waliohusika na vitendo hivyo baadala yake  huficha ukweli na kutoa taarifa za uongo nia na madhumuni wasitiwe hatiani  hali inayopelekea vitendo vya namna hiyo kuota mizizi katika jamii  Mkoani humo. Vilevile ameongeza kuwa Serikali imeboresha zaidi Miundombinu ya  Sekta ya Elimu kama vile  huduma ya  elimu bure,   ujenzi wa  vyumba vya madarasa,  Nyumba za walimu, sambamba na kuongeza kiwango cha ajira za walimu,  lengo ni kuhakikisha kila Mtoto anapata elimu inavyotakiwa, ambapo amewasihi watu wa makundi yote ya  jamii kupitia nyanja zote za   Viongozi wa Serkali, Dini, Siasa,  Asasi za Kiraia,  kuhusika kwa kila namna yake  kupiga vita  dhidi ya vitendo hivyo hususani Wazazi wenye tabia ya kuwaficha wanaume wanaohusika kuwaaribia maisha watoto wa kike  "amesisitiza Katibu Kamugisha.


0 Comment: