KAMATI YA UTEKELEZAJI YA UMOJA WA VIJANA CCM MKOA WA MWANZA YAENDELEA NA ZIARA WILAYA YA KWIMBA

KAMATI YA UTEKELEZAJI YA UMOJA WA VIJANA CCM MKOA WA MWANZA YAENDELEA NA ZIARA WILAYA YA KWIMBA

Leo tarehe 18/06/2019 kamati ya Utekelezaji ya umoja wa Vijana Ccm Mkoa Mwanza
 ikiongozwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Ccm Comredi Jonas Lufungolo  wamefanya ziara katika Wilaya ya Kwimba na Kukutana na Wajumbe wa mabaraza ya kata ya Uvccm Wilaya ya Kwimba Katika muendelezo wa Ziara ya Mkoa wa Mwanza.

Ziara hiyo imelenga Kukutana na mabaraza yote Ya Kata katika maeneo yao husika

Akiwa katika Baraza Hilo Comredi Lufungulo amewataka vijana wote Wawe wazalendo wa Taifa lao kwa Kumuunga mkono Mh  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuri kwa Miradi yote inayotekelezwa kutokana na Ilani ya Chama cha Mapinduzi na wahakikishe wanajitokeza katika fulsa za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa  na kuchukua fomu ili kuleta mabadiliko ndani ya chama na nje ya Chama Kwa kutetea Ilani ya Chama cha Mapinduzi(CCM).

Pia amewasisitiza Vijana wa Uvccm Wilaya ya Kwimba kuwa wajasiri wa kujibu hoja mbalimbali zinazokuwa zinatolewa na watu wanaopinga Maendeleo ya awamu ya Tano.

Amewataka Vijana wa Uvccm Wilaya ya Kwimba kuonyesha Ushirikiano wa Viongozi toka ngazi ya Shina, Tawi, Kata, Wilaya,Mkoa hadi Taifa bila ushirikiano na kushikamana kwa Vijana tutapoze Umoja wetu ulioachwa na Waasisi wa  Nchi Yetu.

Pia Katibu wa Vijana Ccm Mkoa wa Mwanza Comredi DENIS LUHENDE amewataka  Vijana wa Uvccm (W)  Kwimba kuwa Chachu ya Maendeleo kwa Jamii kwa kuanzisha vikundi mbalimbali ili waweze kupata  mikopo yenye riba nafuu na kuweza kuendesha maisha yao bila kutegemea watu na Wawe ndo Dira ya Maendeleo.

Mwisho Comredi Dennis Luhende Katibu Wa Vijana Ccm Mkoa wa Mwanza amewasisitiza vijana wa Uvccm Kitunza na Kuisimamia Amani iliyopo Nchini na kukemea Maovu yote yanayotolewa na vyama vya siasa na watu wasioitakia Mema Nchi yetu ya Tanzania.

Imetolewa na katibu wa hamasa ,chipkizi,Sera na utafiti wa Uvccm mkoa wa mwanza
Hussein A Kimu
Tukutane kazini

0 Comment: