NAIBU WAZIRI MAVUNDE AZINDUA MASHINDANO YA ROMBO DC CUP,AHAMASISHA VIJANA KUFANYA KAZI.


NAIBU WAZIRI MAVUNDE AZINDUA MASHINDANO YA ROMBO DC CUP,AHAMASISHA VIJANA KUFANYA KAZI.








Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde * leo amezindua rasmi Mashindano ya Kombe la DC Rombo,Kilimanjaro itakayoshirikisha Timu *47 kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Rombo ambapo pia ametumia fursa hiyo kuwataka Vijana wa Rombo kufanya kazi kwa bidii kupitia vikundi vya uzalishaji mali ili kujiajiri na kupunguza changamoto ya ukosefu wa Ajira.

Mashindano hayo yameanzishwa na kusimamiwa na Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mh Agness Hokororo ambaye alieleza bayana kuwa madhumuni makubwa ya mashindano haya ni kuendeleza Michezo na kuwaunganisha Vijana wa Rombo kushirikiana katika kuiletea maendeleo wilaya ya Rombo na kwamba Wilaya imejipanga kuhakikisha inakuwa karibu  na Vijana na kutatua changamoto zao mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa mitaji.

Akizungumza na umma wa wananchi wa Rombo,Naibu Waziri Mavunde amempongeza Mkuu wa Wilaya Mh Hokororo kwa ubunifu wa kutumia michezo kuhamasisha shughuli za maendeleo na kuwataka Vijana kuwa mstari wa mbele kushiriki shughuli za kiuchumi na kwamba Serikali ipo tayari kuwawezesha kufikia malengo na matarajio yao.

Aidha Naibu Waziri Mavunde pamoja na wadau wa maendeleo wa Wikaya ya Rombo wamenogesha mashindano hayo kwa ahadi ya kutoa jezi seti 16,mipira 16 na Fedha Taslimu Tsh 1,000,000.

Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na Mbunge wa Viti Maalum(Vyuo Vikuu) Mh Esther Mmas*i na *Prof Adolph Mkenda-Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

0 Comment: