Ifahamu jamii ya watu wasiovutiwa kushiriki tendo la ndoa, wala kuwa na hisia za kimapenzi


Ifahamu jamii ya watu wasiovutiwa kushiriki tendo la ndoa, wala kuwa na hisia za kimapenzi


Wakati hakuna takwimu rasmi za idadi ya watu wanaojitambulisha kuwa hivi nchini China, Mwansaikolojia wa Canada Anthony Bogaert anakadiria kuwa kuna 1% miongoni mwa watu wazima Uingereza walio na hali hii.
Kwa takwimu hizo, watafiti nchini China wandhani kuna takriban watu milioni 10.8 wasiokuwa na hisia na ngono China, kutokana na kwamba kuna watu bilioni 1.08 walio na umri wa zaidi ya miaka 20 kwa mujibu wa takwimu za ivi sasa.
jamii ya watu wasiokuwana hisia za ngono China sasa wapo katika majukwa maarufu kadhaa katika mitandao nchini.
Baadhi yao huwasiliana na kushauriana kila mara na wamevumbua msamiati wao.

Kujitambulisha kama mtu asiyekuwa na hisia za ngono

Kwa Diane anayeishi Shanghai na wanawake wengine nchini China wanajitambulisha kuishi na hali hii.
Hii ni tofauti na watu wanaosusia ndoa au ngono, ambao ni kutokana na uamuzi au unaotokana na mtu kuwa na matatizo ya kingono.
Diane ana miaka ishirini na kitu, amesomea Hong Kong, Uingereza na Uholanzi.
Alianza kujitambulisha kuwa mtu asiyekuwa na hisia za ngono baada ya kukutana na mwanamume Mholanzi aliyekutana naye katika chuo kikuu.
Baada ya hapo, alichanganyikiwa kwanini hakupata hisia zozote za kingono kwa jamaa huyo, licha ya kujivinjari jioni hiyo. Ilimfanya akaanza kujitathmini na kuichunguza hali yake katika mitandao.
Ni kupitia utafiti huo ndipo akaligundua neno AVEN — (Asexual Visibility and Education Network) mtandao mkubwa duniani wa jamii ya watu wasiokuwa na hisia za ngono. baada ya kusoma ufafanuzi wake, alihisi ndio hali aliyonayo yeye.

Animation of a family looking at a book about romance

Diane anasema kutokana na kuwa mwanamke wa Kichina, kuwafungukia wazazi wake lilikuw anijambo gumu sana.
Utamduniwa wachina unatilia mkazo na uzito familia, na wazazi hushtushwa pakubwa panakuwana ishara kwamba watoto wao hawatoolewa au hawatozaa, anafafanua.

Shinikizo kutoka juu

Shinikizo la kuolewa na kuzaa watoto lipo pia katika kiwango cha serikali, huku utawala ukizidi kuwa na wasiwasi kuhusu idadi ya watu nchini.
Kuna wasiwasi maalum kwamba ongezeko kubwa la wanaume nchini waliozaliwa baada ya miaka ya 70 kutokana na uavyaji mimba wa kuchagua , huenda wakazidi kutofanikiwa katika kutafuta mke.
” Nimejaribu mara nyingi kuwaambia wazazi wangu. Hatimaye mamangu sasa ananielewa na ameahidi kutonishinikiza kuolewa jambo ambalo halitonipa furaha. Lakini babangu bado anakaidi. Anahisi kwamba nitakapmpata mtu ninayempenda hisia zitanijia,” anasema.
Kuhojiwa na kupuuzwa ni jambo la kawaida miongo mwa watu walio na hali hiyo. wakati kuna utafiti kiasi unaofanywa kuhusu watu wasiokuwana hisia za kigoon China, bado sio wengi wanaoifahamu hali hiyo.
Mtego mkubwa
Lakini Diane ni mojawapo tu ya idadi inayoongezeka ya wanawake wa China wanaokuwana mtazamao mpya kuhusu sio tu ngono na mahusiano, lakini pia thamani ya ndoa na kuzaa.
“Nadhani ndoa sio kwa maslahi ya mwanamke, ni mtego mkubwa,” anasema.
“Iwapo uzazi ungeweza kufanyika pasi tendo la ndoa , basi watu wataweza kufurahia uhuru binafsi zaidi.”
Diane alipoulizwa iwapo atawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi au amewahi kujihisi mpweke amesema ana rafiki wa karibu lakini anaamini kuwa atasalia kuwa peke yake katika maisha yake yaliosalia.
Hilo anasema ni kwasababu itakuwa vigumu kupata mtu mwingine aliye na hali kama yake ambaye watawiana kimapenzi.

Professor Day Wong reads booksHaki miliki ya pichaDAY WONG
Image captionProfessor Day Wong from Hong Kong Baptist University researches asexuality in China

Kwa mujibu wa BBC. Wanawake wasiokuwa na hisia za kimapenzi wanakabiliwa na changamoto katika utamaduni wa China anasema Professor Wong.
Kwa mujibu wa utafiti wa mtandaoni wa mnamo 2015 uliofanyiwa wachina wanaojitambulisha kama watu wasio na hisia za ngono, 80% yao ilionekana kuwa ni wanawake ambao wamesema mpaka au zaidi ya elimu ya chuo kikuu.
katika makundi hayo kwenye mtandao aliyofuatilia Professor Wong, aligundua wanaume waliosema mambo kama “ukishiriki ngono na mimi utajihisi tofuati”.
“Ni aina fulani ya kuwadhalilisha wanawake, fikra kwamba wanaume ndio bora katika kushiriki tendo hilo na kwamba wanaweza kuwafunza wanawake kuwa na hisia za kushiriki ngono,” anasema.

Lugha mpya

Jamiii inaidhinisha lugha na utambulisho wao.
Hutumia neno “zen” lenye maana “kuwa na amani na mazingira lakini sio kuwa na mahusiano ya kimapenzi na watu”.
Famili za “DINK” zinaongezeka China yaani (double income, no kids) – Kipato mara mbili bila ya watoto.
Hili ni neno linalofafanua familia inayopendelewa kwa jamii ya watu wasiokuwa na hisia za kushiriki ngono.
Pamoja na kuidhinishwa kwa lugha na utamaduni mpya kwa jamii hii, majukwa katika mitandao inatoa fursa kwa jamii ya watu wanaosihi na hali hii kuungana na wengine kama wao kwa mara ya kwanza.
Guo Xu anakumbuka kukutana na mwanamume akiwa katika chuo kikuu aliyemueleza kuwa hana mtu wa kumtegemea kuhusu hali yake. “Niliguswa sana na alichoniambia kwasababu nadhani ndicho wanachohisi wengi walio katika hali hii, tunahisi ni kama ni lazima tuiweke hali yetu siri.” Anasisitiza umuhimu wa kufunguka kuhusu hali hii, na kukubalika na wengine.

0 Comment: