KOCHA WA SIMBA AWAPA TAHADHARI WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA, AGUSIA KIBURI
KOCHA WA SIMBA AWAPA TAHADHARI WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA, AGUSIA KIBURI
LEO timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ itakuwa kazini kumenyana na timu ya Burundi kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar wamepewa tahadhari na Kocha wa zamani wa Simba na Dodoma FC, Jamhuri Khiwelo ‘Julio’.
Akizungumza na Saleh Jembe, Julio amesema kuwa wachezaji wanapaswa kuingia uwanjani wakiwa na nidhamu kwa wapinzani wao kwani wakiwadharau wataambulia maumivu.
“Wachezaji jukumu lao kutambua kwamba wapinzani wao wanahitaji pia ushindi ndio maana wamekuja nchini, kazi kubwa inayotakiwa ni kujituma na kupata ushindi wa mapema ili kujiongezea nafasi ya kujiamini.
“Makosa mengi yamekuwa ni kwa upande wa umaliziaji wa nafasi zinazotengenezwa kwa kuwa tutakuwa nyumbani basi mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu ya Taifa,” amesema.
Mchezo wa kwanza nchini Burundi, Stars iliyo chini ya Kaimu Kocha Etienne Ndayiragije ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 leo inakazi ya kutafuta ushindi kusonga mbele hatua ya makundi.
0 Comment: